HAPA NDIPO SIMBA WALIPOTEANA,KIMATAIFA MIPANGO INAHITAJIKA

JANA ulichezwa mchezo wa Ngao ya Jamii kati ya Simba v Yanga na mwisho wa siku mshindi aliweza kujulikana baada ya dakika 90.

Ilikuwa ni lazima mshindi apatikane kwa namna yoyote ile na mwisho wa siku ikawa kama ilivyotokea kwa timu ambayo imetumia makosa ya mpinzani.

Uwanja wa Mkapa ulisoma Simba 0-1 Yanga hivyo kwa sasa furaha ya mashabiki wa Yanga ipo kwenye taji lao la kwanza kwa msimu mpya wa 2021/22 ambao unatarajiwa kuanza kesho.

Hakuna namna Yanga mnastahili pongezi kwa ambacho mmekifanya na inaonyesha kwamba mlikuwa mnadhamira ya kusepa na taji na mwisho wa siku imekuwa hivyo.

Kwa Simba kupoteza mchezo ni sehemu ya mchezo na hilo lipo wazi hakuna namna maisha lazima yaendelee na pale ambapo mmefanya makosa benchi la ufundi nina amini kwamba litafanyia kazi makosa.

Imeanza kuonekana mapema lakini hili inabidi lifanyiwe kazi hasa kwenye upande wa ushambuliaji ambao katika mechi mbili Simba imeonekana ikipata tabu katika kumalizia nafasi ambazo inazitengeneza.

Ikumbuke ile mechi ya kirafiki ambapo Simba ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0 mbele ya TP Mazembe na mwisho wa siku ilikuwa ni maumivu kwa mashabiki wa Simba.

Pia ilikuwa inaonyesha kwamba ile safu ya ushambuliaji haikuwa na makali ambayo yalikuwa yanaonekana kwenye mechi zilizopita na mwisho wa siku Simba ikashindwa kupata ushindi.

Ngoma ilikuwa ngumu pia kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii baada ya kufungwa bao 1-0 dhidi ya Yanga haina maana kwamba haina uwezo basi ni makosa ambayo yanafanyika.

Ikumbukwe kwamba Simba inakazi ya kuiwakilisha Tanzania kimataifa na hapo kazi inapaswa kuwa kubwa zaidi ikiwa hakutakuwa na mipango makini basi Simba itakwama kutinga hata hatua ya robo fainali.

Kikubwa ambacho kinatakiwa kwa sasa ni kila mmoja kuweza kuangalia namna ya kuweza kuboresha makosa ambayo yamefanyika na mwisho wa siku kuacha maisha yaendelee.

Suala la kuanza kumtafuta mchawi ni nani kwa sasa muda wake umeisha jambo la msingi ni kuona kwamba kila mmoja anatimiza majukumu yake.

Kwenye Ligi ya Mabingwa ni muhimu kufanya vizuri ili kuweza kufikia malengo ambayo Simba imejiwekea kila kitu kinawezekana hivyo ni suala la kufanya maandalizi mazuri.

Wachezaji wa Simba ambao ni wapya wote ni wazuri ila tatizo kubwa lipo kwenye uzoefu wa mechi za ushindani na zile za kimataifa kwa upande wa ligi ya ndani ipo wazi ushindani utakuwa mkubwa ila kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika ni muhimu kujipanga zaidi na zaidi.

Yote yanawezekana hakuna haja ya kutafuta mchawi maandalizi mazuri ni muhimu na kufanya kazi bila kukata tamaa.

Pongezi kwa Kennedy Juma, hapaswi kubweteka hasa akiwa ni mzawa ni lazima aongeze nguvu zaidi na kupambana bila kuchoka.

Hakuna namna wazawa wana nafasi kubwa ya kupeperusha bendera ya Tanzania lakini haitakuwa rahisi bila ya kujituma bila kukata tamaa.

Kilichowafanya Simba wakapoteana ni kushindwa kuwa na utulivu katika mchezo wa jana jambo ambalo liliweza kuwafanya wacheze faulo nyingi tofauti na wapinzani wao Yanga ambao walionekana kucheza kwa kujiamini.

Faulo 26 sio mchezo kwa timu aina ya Simba na namna ambavyo imekuwa ikicheza lakini ni mpira na matokeo lazima yapokelewe hakuna anayeweza kuyabadili.

Kwa kadi nyekundu hakuna namna ilikuwa lazima iwe hivyo kwa sababu Taddeo Lwanga aliweza kucheza faulo nyingi kwenye kucheza mpira na mwisho wa siku akaonyeshwa kadi mbili za njano.

Mabadiliko ya lazima hayakuwa na chaguo kwa Kocha Mkuu, Dider Gomes kwa kuwa alilazimika kuwatoa wachezaji wake ikiwa ni Joash Onyango pamoja Kanoute.

Imeandikwa na Dizo Click 

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments