Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes itakuwa Uwanja wa Karume, Mara bila uwepo wa nyota wao Taddeo Lwanga ambaye alionyeshwa kadi nyekundu katika mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga, Uwanja wa Mkapa, Septemba 25.
Mbali na mchezo huo unaosubiriwa kwa shauku kubwa pia Dodoma Jiji itakuwa na kibarua cha kusaka pointi tatu mbele ya Ruvu Shooting, Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.
Pia kuna mchezo mwingine ambapo Mbeya City itakuwa na kibarua cha kusaka pointi tatu mbele ya Tanzania Prisons, Uwanja wa Sokoine.
0 Comments