HIZI HAPA REKODI ZA MWANZO LIGI KUU BARA

SHUGHULI imeanza upya kwa timu za Lifi Kuu Bara kusa ushindi kwenye mechi ambazo wanazicheza ikiwa ni msimu mpya wa 2021/22 na tayari rekodi tamu zimeanza kuandikwa kwenye mechi za ufunguzi.

Mechi ya kwanza kwa msimu wa 2021/22 iliwakutanisha mabosi kutoka Morogoro ambao ni Mtibwa Sugar ilikuwa Uwanja wa Mabatini, Kibaha dhidi ya Mbeya Kwanza ambayo ni msimu wake wa kwanza kushiriki ligi baada ya kupanda daraja.

Katika mechi hiyo iliandikwa rekodi ya kuwa mechi ya kwanza ambayo ilikusanya bao la kwanza dakika ya 49 kwa shuti kali akiwa ndani ya 18 akitumia mguu wake wa kushoto kupachika bao hilo.

Mtupiaji alikuwa ni Willy Edgar na kipa aliyemtungua kwa mara ya kwanza ndani ya ligi ni kipa namba moja wa Mtibwa Sugar ni Aboutwalib Mshery ambaye kwa msimu wa 2020/21 alikusanya jumla ya clean sheet 14.

Mbali na rekodi hiyo iliyowekwa ndani ya dakika 90 kwenye mchezo wa kwanza pia kuna rekodi nyingine ambayo iliwekwa na nyota wa Namungo FC, Obrey Chirwa kuwa ni namba moja kwa kutengeneza pasi nyingi kwenye mchezo mmoja.

Alitoa jumla ya pasi mbili kwa waskaji zake wawili tofauti na zote alitumia mguu wake wa kulia kutoa pasi hizo ilikuwa Uwanja wa Ilulu, Lindi.

Kwenye mchezo huo Namungo FC inayonolewa na Kocha Mkuu, Hemed Morocco iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Geita Gold ambayo imekaribishwa kwenye ligi kwa kuyeyusha pointi tatu mazima.

Alitoa pasi yake ya kwanza kwa mshikaji wake Shiza Kichuya ilikuwa ni dakika ya 13 ambaye alifunga bao kwa shuti kali akiwa ndani ya 18 na pasi ya pili alitoa kwa mshikaji wake Reliat Lusajo ambaye alipachika bao hilo dakika ya 80 kwa mguu wa kulia na Chirwa alikuwa nje ya 18 wakati akitoa pasi hiyo mpenyezo.

Pale Mkwakwani ilikuwa ni vurugu mechi baada ya dakika 90, ubao kusoma Coastal Union 1-1 Azam FC ambapo mabao yote yalifungwa na wafungaji kwa mtindo mmoja ilikuwa kwa kutumia kichwa na walikuwa ndani ya 18.

Alianza Daniel Amoah kupachika bao dakika ya 82 lilisawazishwa na Hance Masoud dakika ya 89 na kufanya timu hizo kugawana pointi mojamoja.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments