INTER PORTS GAMES YAENDELEA KUTIMUA VUMBI MJINI MOROGORO.

 Mashindano ya Bandari maarufu kama Inter ports Games yameanza kutimua vumbi Mkoani Morogoro katika viwanja vya mpira wa miguu jamhuri na uwanja wa kikapu wa JKT Bwalo la umwema vya Mjini Morogoro, yakishirikisha wanamichezo zaidi ya mianne (400) kutoka katika bandari zote ikiwemo bandari za maziwa makuu huku timu ya bandari ya Dar Es Salaam ikiibuka mshindi kwenye mchezo wa kuvuta kamba.


Akizungumza katika ufunguzi wa michezo hiyo Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Bwana Albert Msando,amezitaka timu zote zilizo shiriki katika mashindano hayo kuwa na ushindani na sio kushiriki.

Pamoja na kushiriki katika michezo hiyo mkuu wa wilaya huyo amewataka wanamichezo kuchukua tahadhari juu ya maswala ya afya hususani katika ugonjwa wa Covid 19 na virusi vya ukimwi. Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TPA Bwana Erick Hamissi amesema kuwa TPA inatambua umhimu wa michezo katika kuimarisha afya za wafanyakazi.

Amesema Katika mashindano haya ambayo yanafanyika kwa siku nane mjini Morogoro yatashirikisha mchezo wa mpira wa miguu, mpira wa pete, mpira wa kikapu, kuvuta kamba mchezo wa bao pamoja na mchezo wa riadha.

Aidha amewataka wanamichezo walioshiriki katika michuano hiyo kutumia siku 8 watakazokuwa mjini Morogoro kutumia michezo kudumisha mahusiano mema kazini pamoja na wadau wa TPA.

“Lakini tutumie michezo hii kujitangaza kimasoko kwa wadau wetu na kuhimarisha utendaji kazi wa taasisi zetu,pia naomba kila mmoja wetu awajibike ipasavyo ili kuhakikisha malengo ya taasisi yanafikiwa.”Alisema Mkurugenzi wa TPA Bwana Erick Hamissi.

Kwa upande wao wachezaji wa mchezo wa kuvuta kamba wa timu za bandari ya Tanga na Dar Es Salaam ambao ndiyo wamefungua mashindano haya wamesema michezo inasaidia kuimarisha afya ya mwili na kudumisha mahusiano manzuri kazini.





                               NA FARIDA SAIDY,MOROGORO.


TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments