Recent-Post

JERRY MURRO KUTUMIA MITANDAO KUTATUA KERO ZA WANANCHI

 Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Jerry Muro amesema ili kutatua jero za wananchi wa wilaya ya Ikungi atatumia kurasa za mitandao ya kijamii, face book, instagram na Twitter pamoja na makundi ya whatsapp ili kujua kero zao na kuzitafutia utumbuzi.

Muro amesema hayo katika mkutano wake na wa awamu ya kwanza na wananchi wa kata ya Unyaahat kijiji cha mahambe jimbo la singida mashariki wilaya ya Ikungi.

Aidha amesema ili kuyafikia makundi mengi atatumia pia atatumia mfumo wa kuweka taarifa kwenye ofisi za serikali za vijiji kupitia watendaji wa vijiji na kata,  mikusanyiko katika madhehebu ya dini na  mikutano ya hadhara itakayofanywa na viongozi wa kisiasa wabunge, madiwani na wenyeviti wa vijiji.
                                    Singida Ikungi

Post a Comment

0 Comments