JUKWAA la Wanawake Wilaya Mkuranga mkoani Pwani wamemchagua Mariam Ulega kuwa Mwenyekiti wao baada ya kuibuka na ushindi wa kura 99 dhidi ya kura saba alizopata mshindani wake.
Akizungumza baada ya kutangazwa kushinda nafasi ya Mwenyekiti wa Jukwaa hilo,Mariam Ulega ameahidi kufanya kazi za kwa bidii,juhudi na maarifa na kwamba hatawaangusha wanawake wa Mkuranga.
"Nitahakikisha nashirikiana wananchi wote wa Mkuranga katika kuendelea kuleta maendelo .Nitahakikisha nasimama imara katika kuifanya Wilaya yetu inapaa kimaendeleo,"amesema Mariam Ulega.
Amewaomba wanaweke ambao hawana vikundi wavianzishe na kisha wavisajali na hatimaye kukopeshwa fedha ambazo hazina riba kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga, na hivyo wataweza kuinuka kiuchumi kwa kufanya shughuli mbalimbali.
Mbali ya kutoa shukrani kwa wapiga kura wa jukwaa hilo,Mwenyekiti huyo amesema Jukwaa hilo la Wanawake Mkuranga wamepokea Cherahani saba kutoka kwa Mbunge wa Jimbo la Mkuranga,Abdallah Ulega.
"Leo tumepolea Cherehani saba kutoka kwa Mbunge , ni vema tuzitunze na zifanye kazi iliyokusudiwa ya kushona nguo za watoto wa shule , uwepo wa Cherehani hizo zitawezesha wakina mama wa Mkuranga tusonge mbele,"amesema.Mwenyekiti wa Jukwaa la Wanawake Wilaya ya Mkuranga,Mariam Ulega akizungumza na wapigakura baada ya kutangazwa kushinda nafasi ya Mwenyekiti wa Jukwaa hilo, ambapo ameahidi kufanya kazi kwa bidii,juhudi na maarifa na kwamba hatawaangusha wanawake wa Mkuranga.Uchanguzi huo umefanyika leo kwenye ukumbi wa Parapanda Wilaya ya Mkuranga Mkoani wa Pwani.(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi TV)
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wanawake Wilaya ya Mkuranga,Mariam Ulega (kushoto) akimkabidhi Cherehani Makamu Mwenyekiti wa Jukwaa hilo.
0 Comments