KAPOMBE AONDOLEWA KIKOSINI SIMBA

 

SIMBA imevimba na usajili mpya wa beki wa kulia, Israel Mwenda ambapo kauli ya Kaimu Msemaji wa Simba Ezekieli Kamwaga, imeanika kwamba tayari usajili wake umeonekana kulipa kwa Didier Gomes, ambapo sasa amelazimika kumweka kando staa wake, Shomari Kapombe, na kutoa fursa kwa kinda huyo.

 

Msimu uliopita, Gomes alionekana kukosa mbadala sahihi wa Kapombe na kulazimika kila mara kumtumia katika kila mechi, baada ya David Kameta ‘Duchu’, kushindwa kuonyesha upinzani aliokuwa akiuhitaji jambo ambalo sasa limezibwa na kinda huyo kutoka KMC.

 

Taarifa ya Kaimu Msemaji wa Simba, Ezekiel Kamwaga imelijuza Championi Jumatatu kwamba ni wazi sasa kocha wao Gomes ameshusha pumzi yake baada ya kufanikiwa kupata mbadala sahihi wa Kapombe, jambo ambalo mwanzo lilikuwa likimnyima usingizi.

 

“Mashabiki wetu wengi awali walikuwa hawaamini katika usajili wetu wa vijana wenye umri mdogo tuliowapa nafasi msimu huu, ila kiukweli kwa benchi la ufundi sasa hivi linachekelea tu baada ya sajili hizi kuonyesha matunda hasa ukianza na safu ya ulinzi wa kulia, ambapo tumemuongeza Mwenda.

 

“Mwenda ana kiwango bora sana kiasi kwamba amemshawishi kocha, hadi hawazi tena kuhusu Kapombe hata akiumia kama ilivyokuwa mwanzo,” alisema Kamwaga

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments