KATIBU MKUU CCM: NFRA ACHENI KUHIFADHI HELA ZA WAKULIMA KWENYE MIFUKO YENU

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Ndg. Daniel Chongolo amewataka Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA), kuchangamka kununua mahindi kwa wakati ili kuwafanya wakulima kuendelea na shughuli zao za maendeleo.

Katibu Mkuu ameyasema hayo Ruvuma wilayani Mbinga wakati akiongea na wananchi na wanachama wa Chama hicho wakati wa ziara ya wajumbe wa  Sekretariet ya Halmashauri kuu ya CCM Taifa.

Ambapo  amesema, tayari Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ametoa fedha shilingi bilioni 50 kwa ajili ya Ununuzi wa mahindi hayo kwa wakulima kwa awamu ya pili.

Katibu Mkuu amesema, Rais Samia ametoa fedha za kununulia mahindi ni lazima watu wa NFRA waweze kuchangamka  kwani kazi ya fedha sio kukaa katika mifuko au akaunti za Taasisi, kazi yake ni kuelekea kwenye maeneo  yaliyokusudiwa.

"Mwananchi amelima shamba lake kwa bidii, kavuna vizuri mazao yake  anataka  kutengeneza mambo yake na anataka kujipanga na pembejeo za msimu ujao  wakicheleweshwa kwenye mambo ya Msingi watakuwa hawatendewi haki." Katibu Mkuu

"Sisi tufanye kazi yetu ya singi tununue mahindi kwa wakati,mahindi yakishanunuliwa Mwananchi  atajipangia mwenyewe manunuzi yake kwa sababu fedha ni ya kwake mwenyewe," Katibu Mkuu amesisitiza

Katika hatua nyingine, Katibu Mkuu amewaomba wananchi wa Mbinga kulima mazao mengine ambayo yanastahimili  kwenye eneo la mkoa huo ili kuendeleza kupanua wigo wa mzunguko wa kipato.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments