KATIBU MKUU WA CCM NA SEKRETARIETI YA HALMASHAURI KUU YA TAIFA KUANZA ZIARA YA KIKAZI MIKOA YA LINDI,MTWARA,RUVUMA NA NJOMBE.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg. Daniel Chongolo atakuwa na Ziara ya Kikazi Mikoa ya Lindi, Mtwara, Ruvuma na Njombe akiambatana na Wajumbe wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa.

Ziara hiyo itaanza tarehe 15 - 21 Septemba, 2021 Mkoani Lindi katika Wilaya zote za Mkoa huo, na kuendelea katika Mikoa ya Mtwara, Ruvuma na kumalizia Mkoani Njombe.

Malengo ya ziara hiyo ni kuimarisha Uhai wa Chama katika ngazi za Mashina pamoja na Kukagua Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020 - 2025, ikiwa ni Utekelezaji wa Maelekezo ya Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa cha  tarehe 29 Juni, 2021.

Wajumbe wa Sekretarieti watakaojumuika katika Ziara na Katibu Mkuu ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM - Bara Ndg. Christina Mndeme, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Ndg. Shaka Hamdu Shaka, Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Ndg. Ngemela Lubinga, Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM Ndg. Kennan Kihongosi, Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake Dkt. Philis Nyimbi na Katibu Mkuu wa Umoja wa Wazazi Ndg. Gilbert Kalima.

Imetolewa na;

Said Said Nguya
Afisa Habari
Ofisi ya Katibu Mkuu
CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)
14 Septemba, 2021

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments