Recent-Post

KATIBU MKUU WA UVCCM AENDESHA HARAMBEE YA UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI KATA YA UPINZANI.

Rais  Mhe.Samia Suluhu Hassan  na Serikali yake ya awamu ya sita mbali na kuendelea kutoa elimu bure,serikali ya awamu ya sita inaendelea kujenga shule sehemu mbalimbali na kuelendelea kufanya mapinduzi kwenye sekta hii na ndio maana nimeendesha harambee ya ujenzi wa shule ya Sekondari Mkunwa na tumefanikiwa kupata mifuko ya saruji 370,tofali 1800 pamoja mchanga lori 3 pamoja na kata hii kuwa ipo Chini ya upinzani na Hongera sana Diwani kwa kutambua mchango mkubwa wa CCM na kuamini maendeleo yanapatikana CCM pekee.


Serikali ya CCM imeshusha umeme mpaka elfu 27,000/= tuu na nguzo ni bure,Mh.Rais amedhamiria mpaka 2025 kila nyumba iwe inawaka Umeme.

Serikali ya awamu ya sita inaendelea kuleta maendeleo kwenye kila pembe ya Nchi yetu,imeleta hapa kwenye kijiji cha Mkunwa ml.250 kwaajili ya kituo cha Afya pamoja na kwamba kata hii ipo Upinzani.Wabunge kote nchini wamepewa fedha kwaajili ya barabara,vituo vya afya pamoja na maji.Kazi inayofanywa ni kubwa tuendelee kumuombea Rais wetu.

Mwakani kuna Sensa ya watu na makazi,,nawahamasisha wananchi wenzangu wa hapa Mkunwa na kote nchini kujitokeza kwa wingi kuhesabiwa,kwani ni lazima serikali ijue idadi ya watu wake ili ijue inapeleka wapi maendeleo kwa kasi zaidi.

Katibu Mkuu aliwasihi wananchi kuendelea kumuunga mkono Mh. Rais kwani dhamira yake kwa Taifa letu siyo yakutiliwa mashaka

*KAZIIENDELEE
MTUMISHIWAWOTE*

Post a Comment

0 Comments