KESI ya tuhuma ya ugaidi inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo( Chadema)Freeman Mbowe na wenzake watatu inatarajia kuanza kusikilizwa Septemba 15, 2021 katika Mahakama Kuu kitengo cha makosa ya Uhujumu Uchumi na Rushwa maarufu kama Mahakama ya Mafisadi.
Hatua hiyo imekuja baada ya leoSeptemba 10, washtakiwa hao kusomewa maelezo ya awali.Katika kesi hiyo upande wa mashtaka unatarajiwa kuita mashahidi 24 na vielelezo 19 ili kuthibitisha mashtaka dhidi ya washtakiwa huku upande wa utetezi ukitarajiwa kuwa ma mashahidi 11.
Mapema akisoma maelezo ya awali,Wakili wa Serikali Tulumanywa Majigo amedai mshtakiwa wa kwanza, wapili na watatu wote walikuwa waajiriwa wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), walioudhulia mafunzo ya ukomandoo katika kambi ya Ngerengere Mkoani Morogoro na waliofukuzwa kazi kutokana na vitendo vya utovu wa nidhamu.
Majigo amedai kuwa washtakiwa hao watatu wanafahamiana huku mshitakiwa wa nne (Mbowe) akiwa ni Mwenyekiti wa Taifa wa chama cha siasa cha CHADEMA.
Wakili huyo amedai washitakiwa wote wanne wanakabiliwa na mashtaka mawili ya kula njama, mshitakiwa wa kwanza na wapili wanashtakiwa na makosa ya kukutwa na mali iliyokusudiwa kutumika kutenda vitendo vya kigaidi huku mshitakiwa wa nne pekee akikabiliwa na shitaka la kutoa fedha kwa ajili ya kufadhilii vitendo vya kigaidi.
Majigo amedai Kwamba Julai mwama 2020 mbowe Aliomba Kukutana na Luten Denis Urio ambaye walikuwa wanafahamiana awali.
Waliafikiana kukutana na baadae walikutana katika moja ya mgahawa uliopo maeneo ya mikocheni na wakiwa katika eneo hilo Mbowe alimuomba Luten amtafutie Makomando waliofukuzwa kazi ili wamsaidie katika kutekeleza vitendo vya kigaidi ambavyo ni kulipua vituo vya mafuta mikusanyiko ya umma katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Dar es salaama, Mwanza na Arusha.
Wakili ameendelea kudai kuwa Mbowe alimweleza Luteni Hurio lengo la kutaka kufanya hivyo ni kuleta taharuki kwa wananchi na kuharibu misingi iliyopo nchini kisiasa na kiuchumi.
Imeendelea kudaiwa kwamba, Mbowe alitoa Sh Laki 699,000 ili kuwezesha makomando aliotafutiwa ambao kwa sasa ni washtakiwa wenzake kuja Dar es Salaam ili kupanga namna ya kutekeleza ugaidi huo.
Inadaiwa kuwa Mbowe alikuwa akiwasiliana na wenzake kupitia mitandao ya Telegrama na kabla ya kukutekeleza kitendo hicho washtakiwa walikamatwa.
Ameeleza kuwa mshtakiwa Adam Kusekwa Mohamed Lingwenywa walikamatwa eneo la Rau wakiwa katika harakati za kumsababishia Sabaya majeraha na mshita pili alipopekuliwa alikutwa na siraha aina ya Pisto yenye Pastola tatu ambazo zilikuwa na nia ya kutumika katika vitendo hivyo.
Washitakiwa hao walisafirishwa hadi Dar es Salaam na walipohojiwa walikiri kujihusisha na vikao mbalimbali vya kigaidi na walimtaja mshtakiwa Khalfan Bwire na Mbowe kuwa sehemu ya wahalifu.
Agosti,9 mwaka 2020 mshitakiwa Hassan Bwile , alikamatwa eneo la Changa'ombe na walipohojiwa katika kituo cha polisi Chang'ombe alikiri kuhusika katika kikao cha kutekeleza vitendo vya kigaidi.
Wakili amedai mshitakiwa Bwile alipopekuliwa katika makazi yake eneo la Yombo alikutwa na mali za Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) pamoja na kidaftari kidogo na baada ya upekuzi fomu ya upekuzi ilidaiwa na kushikwa mshitakiwa
Amedai kuwa kidaftari hicho kilipopelekwa katika maabara ya maandishi ilibainika kuwa mwandiko ulikuwa katika daftari hilo ni sawa na mwandiko wa mshitakiwa huyo.
Pia Agosti 11 mwaka 2020 Luteni Urio aliwasilisha simu yake aina ya Tecno katika maabara ya makosa ya mtandao kwa ajili ya uchunguzi na kuaminika kwamba meseji za mawasiliano zilizokuja katika mtandao wa Telegram kati Mbowe na Urio zilipatikana katika simu hiyo.
Amedai Jeshi la Polisi liliendelea na uchunguzi na Julai 20 mwaka huu Mbowe alikamatwa Mtaa wa Ghana ,Mwanza na kuunganishwa na washitakiwa wenzake ambao ni Bwire Kasekwa na Lingwenya
Baada ya kusomewa maelezo hayo, washitaliwa hao kupitia wakili wao Kibatala, mshtakiwa wa kwanza, wapili na watatu walikubali majina yao na anwani zao.
Pia washtakiwa hao wamekubali walikuwa watumishi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania kama Makomandona na Ajira zao zilisitishwa kwa sababu ya vitendo vya utovu wa nidhamu.
Washitakiwa hao wamekiri kufanya kazi pamoja katika kikosi cha Jeshi Ngerengere mkoa wa Morogoro na kwamba wanafahamiana.
Kwa upande wa mshtakiwa Freeman Mbowe), amekubaliana na majina na anwani yake ya makazi na kwamba ni Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema.Mbowe amekiri kukamatwa Mtaa wa Ghana ,Iremela Mkoani Mwanza.
Awali Wakili wa Utetezi Peter Kibatala alitaja kwa majina mashahidi saba pekee huku wengine wanne akiomba mahakama kutoa kibali kwani baadhi yao ni maafisa wa polisi na hivyo wanaweza kufikiwa kabla ya kutoa ushahidi wao mahakamani hapo ombi ambalo limepingwa na upande wa Jamhuri.
Hata hivyo, Jaji Siyani amesema, amesikiliza hoja za pande zote mbili amekubaliana na ombi la kibatala licha ya kuwa sheria hairuhusu ila inatoa mamlaka kwa mahakama kutoa uamuzi endapo kunakuwa na mazingira yanayolazimisha mashahidi kufichwa.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Spetembe15 kwa ajili ya Kuanza kusikiliza mashahidi wa upande wa Jamuhuri.
0 Comments