Recent-Post

Kinyozi maarufu Mirerani mbaroni kwa tuhuma za kumlawiti bubu

Mirerani. Kinyozi maarufu wa Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, Athuman Rashid (57) anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kumlawiti kijana mwenye ulemavu wa kusikia na kuongea.

Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Manyara, Merrison Mwakyoma akizungumza na Mwananchi Digital leo Septemba 9, amesema tukio hilo lilitokea juzi mtaa wa Tunduru katika mji huo.

Kamanda Mwakiyoma amesema Athuman alikamatwa na wananchi akiwa anamlawiti mvulana huyo wa miaka 21 (jina lake linahifadhiwa) kwenye kibanda usiku wa tukio hilo.

Amesema mama wa kijana huyo aliambiwa na baadhi ya majirani wa eneo hilo kuwa mtoto wake huwa analawitiwa na Athuman ndipo wakaenda polisi kutoa taarifa.

Mshtakiwa alikamatwa akiwa anamlawiti kijana huyo na tunaendelea na uchunguzi wa tukio hilo kabla ya kumfikisha mahakamani kwa ajili ya kusomewa mashtaka,” amesema kamanda Mwakyoma.

Ametoa onyo kwa wananchi kujihusisha na matukio ya aibu kwenye jamii kama hili kwani tabia za laana kama hilo halifai na amewapongeza wananchi waliofanikisha kukamatwa kwa mtuhumiwa.

“Mungu ameweka utaratibu wa kibinadamu katika kujamiiana hata wanyama hawafanyi hivi, tumejiandaa na ushahidi ikiwemo taarifa ya daktari ili aweze kuadhibiwa na mahakama,” amesema kamanda Mwakyoma.

Post a Comment

0 Comments