Recent-Post

MAJALIWA AMPOKEA NA KUMKABIDHI KADI YA CCM ALIYEGOMBEA UBUNGE JIMBO LA KASULU VIJIJINI KADA WA CHAMA CHA ACT-WAZALENDO

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmshauri kuu ya Chama cha Mapinduzi na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa jana Septemba 16, 2021 amempokea kada wa Chama cha ACT-Wazalendo  aliyekuwa mgombea wa ubunge katika jimbo la Kasulu vijijini Adibily Kazala


Akizungumza baada ya kupokea kadi ya CCM  wakati wa Kikao cha Halmashauri kuu ya CCM mkoa wa Kigoma Bw. Edibily amesema kuwa ameamua kujiunga na CCM ili kuweza kushikiri kikamilifu katika ujenzi wa taifa kwa kuunga mkono juhudi mbalimbali za kuleta maendeleo zinazotekelezwa na Serikali ya Chama cha Mapinduzi.

Amesema kuwa atashirikiana na wanachama wa CCM katika kuhakikisha juhudi za kuwafikishia watanzania maendeleo zinatekelezwa kama ilivyokusudiwa na Chama hicho.

Naye Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Kassim Majaliwa amewakumbusha viongozi wa Chama hicho kufuatilia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo kama ilivyoelekezwa katika ilani ya uchaguzi ya chama hicho


 

Post a Comment

0 Comments