Recent-Post

Manara afunguka

 

MCHEZAJI wa zamani wa Yanga, Sunday Manara amesema ili kikosi cha Yanga kiweze kufanya vizuri katika michuano ya Ligi ya Mabingwa na Ligi Kuu kinahitaji maandalizi ya kutosha ikiwemo mechi za kujipima nguvu.

Licha ya kupoteza mabao 2-1 dhidi ya Zanaco kwenye siku ya Mwananchi, alisema kwa namna ambavyo Yanga walicheza wanahitaji kupata mechi nyingi ambazo zitaijenga zaidi timu iwe yenye ushindani zaidi.

Alisema kwa namna ambavyo walikuwa hawajajipanga wamepata kitu kucheza na Zanaco na hata kocha wao Nasreddine Nabi atakuwa amepata kitu kupitia mchezo huo.

Na kuhusu mwanaye Haji Manara kuhamia Yanga kutoka Simba alisema amefanya hivyo kutokana na baadhi ya viongozi wa Simba kutothamini alichokuwa akikifanya na amefanya hivyo kwa hasira kama mwanadamu mwingine yeyote.


Post a Comment

0 Comments