Recent-Post

MANCHESTER UNITED YANYOOSHWA NA RONALDO WAO

 

LICHA ya nyota wao Cristiano Ronaldo kupachika bao la ufunguzi dakika ya 13 katika mchezo wa UEFA Champions League wakiwa kundi F, bado Manchester United iliyeyusha pointi tatu mazima katika mchezo huo.

Pia Ronaldo ameweza kuingia katika rekodi ya wachezaji waliocheza mechi nyingi za UEFA akifikisha jumla ya mechi 177 sawa na Iker Casillas.

Baada ya dakika 90, ubao wa Stade de Suisse uliokusanya jumla ya mashabiki 31,120 ulisoma Young Boys 2-1 Manchester United huku watupiaji wa Young Boys wakiwa ni Moumi Ngamaleu ilikuwa dakika ya 66 na lile la ushindi lilifungwa na T.Siebatcheu dakika ya 90.

Nyota wa Manchester United,  Wan-Bissaka alionyeshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja dk 35 na anakuwa mchezaji wa kwanza wa timu hiyo kuonyeshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja katika mashindano ya UEFA tangu mara ya mwisho iwe hivyo mwaka 2013 Machi ilikuwa ni kwa Nani dhidi ya Real Madrid.

Post a Comment

0 Comments