MSAJILI AIPONGEZA CCM KUJIENDESHA KITAASISI

Katiubu Msaidizi Mkuu Oganizesheni ya Chama cha Mapinduzi, Ndg. Solomon Itunda akimkabidhi nyaraka za chama Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa, Bw. Sisty Nyahoza wakati wa zoezi la uhakiki wa namna chama hicho kinavyotekeleza sheria ya vyama vya siasa na sheria ya gharama za uchaguzi leo jijini Dodoma.




Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa, Sisty Nyahoza akizungumza wakatiu wa zoezi la Uhakiki katika Ofisi za Makao Makuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) jijini Dodoma



Katibu wa Sekretarieti ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Ndg. Salum Reja akizungumza wakati wa zoezi la a na hakiki lililoendeshwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa katika Ofisi za Makao Makuu ya chama hicho jijini Dodoma



Afisa Tehama wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Bi. Levina Myovela akitoa maelezo mbele ye wajumbe kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa (ORPP) namna CCM inavyotumia mifumo ya Tehama katika uendeshaji wa shughuli zake jijini Dodoma



Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa (ORPP), Bw. Peter Lyimo (kushoto) akiwa pamoja na Msaidizi wake Bw. Mussa Boma wakikagua kitabu cha hesabu za Chama cha Mapinduzi wakati wa zoezi la uhakiki wa namna vyama vya siasa vinavyotekeleza Sheria zinazosimamiwa na Ofisi ya Msajili katika Ofisi za Makao Makuu ya chama hichi jijini Dodoma



Wajumbe kutoa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa (ORPP) wakifuatilia zoezi la uhakiki walipotembela Ofisi za Makao Makuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) jijini Dodoma


Baadhi ya watendaji wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Makao Makuu wakifuatilia zoezi la uhakiki wa namna vyama vya siasa vinavyotekeleza Sheria zinazosimamiwa na Ofisi ya Msajili walipotembela Ofisi za Makao Makuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) jijini Dodoma



Watumishi kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa (ORPP) wakiongozwa na Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa, Bw. Sisty Nyahoza (mwenye tai) wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Makao Makuu jijini Dodoma leo. (Picha zote na: ORPP)

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments