Recent-Post

MwananchiHabari ZaidiKitaifa DC Kiswaga ashtukia utoroshaji wa madini, akamata wachenjuaji 10

Wamiliki 10 wa mialo ya kuchenjua madini ya dhahabu wilayani Kahama wanashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kutokutumia vitabu vya kutunza kumbukumbu za uchenjuaji wa madini.

Amri ya kutiwa mbaroni kwa wamiliki hao ambao pia wanadaiwa kuuza madini kwa njia ya magendo imetokewa leo Septemba 26 na Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Festo Kiswaga alipofanya ziara ya kyshtukiza ya kukagua shughuli za uchenjyaji katika mialo hiyo.

DC Kiswaga pia amemwagiza kaimu Ofisa Madini mkoa wa kimadini wa Kahama, Jeremia Hango kukagua vitabu vya kumbukumbu za utunzaji wa taarifa za madini katika mialo yote wilyani humo na kuwachukulia hatua za kisheria wamiliki wote watakaobainika kukiuka kanuni na taratibu za kusheria.

Nimeagiza wamiliki hawa 10 watozwe faini kwa mujibu wa sheria za madini na wengine watakaobainika kukiuka sheria kwa makusudi. Hatutatoa nafasi ya kulipa faini na badala yake tutawapeleka mahakamani kwa makosa ya uhujumu uchumi,” amesema Kiswaga.

Alisema aliamua kufanya ziara ya kushtukiza kukagua shughuli za uchenjuaji na uuzaji wa dhahabu baada kuwepo taarifa za biashara ya madini hayo kushuka wilayani humo.

"Uuzaji wa madini kwenye masoko yetu imeshuka lakini uzalishaji bado upo juu. Mwezi uliopita masoko yetu yaliuza dhahabu yenye kilogramu 25, kumbe kuna watu wameanza kutumia njia zisizo rasmi kutorosha madini. Lazima tuwe macho kudhibiti hali hiyo," alisemaKiswaga.

Kaimu Ofisa Madini mkoa wa Kimadini Kahama, Jeremia Hango ameahidi kuwa ofisi yakr itatekeleza agizo maagizo yoye ya mkuu wa wilaya huku akiwataka wachimbaji na wafanyabiashara kujiepusha na vitendo vinavyokiuka sheria.

Mwenyekiti wa wachimbaji wa madini ya dhahabu Wilaya ya Kahama, Joseph Nalimi ameiomba serikali kuwapatia vifaa na elimu ya utambuzi wa miamba ili kuepuka uchimbaji wa kuhamahama ambao unachangia kuharibu mazingira.

Post a Comment

0 Comments