Recent-Post

MWENDOKASI YAUA WAWILI DAR

 

WATU wawili wamefariki dunia kwa ajali iliyohusisha basi la Mwendokasi na Pikipiki katika  barabara ya magari ya mwendokasi Lumumba jijini Dar es Salaam.

Akithibitisha kutokea kwa ajili hiyo leo Jijini Dar es Salaam Kamanda wa Jeshi la polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amesema kuwa  ajali hiyo ilitokea  Agosti 08 majira ya saa 21:20 usiku katika barabara ya mwendokasi eneo la Lumumba kwenye taa za kuongozea magari,ambapo pikipiki yenye namba za usajili MC 663 CDX aina ya Boxer ikiendeshwa na Sami Riyaz Khan(17),Mkazi wa Gerezani, akiwa na abiria wake Patrick Chohan(16) iligongana na basi la mwendokasi lenye namba za usaji T 880 DGV aina ya Golden Dragon lililokuwa likitokea Kimara kuelekea Kivukoni na kusababisha vifo vya dereva wa pikipiki na abiria.

Kamanda Muliro   amesema kuwa Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa chanzo cha ajali ni dereva wa pikipiki kujaribu kupita taa nyekundu kinyume cha sheria, ndipo walipogongwa na gari la Mwendokasi na kufariki dunia wote.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam linawataka madereva wa pikipiki kutii sheria za usalama barabarani husasani taa za kuongozea magari,kuvaa kofia ngumu na kutopita kwenye barabara za Mwendokasi.

Post a Comment

0 Comments