Ndugai ahoji ripoti ya mawaziri wanane

 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi amesema kwa sasa hana jipya la kuzungumzia kuhusu ripoti ya kamati ya mawaziri wanane iliyoundwa kuchunguza migogoro ya ardhi hadi hapo watakapokamilisha kazi waliyopewa na Rais Samia Suluhu Hassan.

Sakata hilo limeibuka wakati wa kipindi cha maswali na majibu leo Jumanne Septemba 7, 2021 ambapo Spika Ndugai alimuuliza Lukuvi endapo ripoti hiyo imefikia kiwango cha wabunge kufahamu.

Akijibu Lukuvi amesema leo asubuhi uliunda kamati mbili kwenda kushughulikia jambo hilo ambalo Rais (Samia Suluhu Hassan) ametupa maelekezo mwezi uliopita.


Amesema aliziambia kamati hizo kwa sasa hawana jipya na kwamba wanasubiri kazi ya kwenda kufanya uhakiki wa kina.
“Kwa sababu maamuzi haya yamefanyika miaka mitatu iliyopita, ametutuma hatutakuwa na kusema hadi (uhakiki) utakapokamilika wa uandani huu,”amesema.

Soma hapa:Ndugai atishia kuifumua kamati ya Bunge ya Bajeti

Amesema watafika mikoani na huko watakutana na wabunge ambao watachukua maelezo yao baada ya kukamilika na mheshimiwa Rais kutolea maamuzi tutakuja kutoa taarifa tena.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments