Recent-Post

NYOTA SABA KIKOSI CHA KWANZA KUUZWA NA MANCHESTER UNITED

KLABU ya Manchester United imetajwa kuwa ina mpango wa kuuza nyota wake saba ifikapo Januari mwakani. 

Nyota hao saba wote wanatoka katika kikosi cha kwanza cha Man United sababu za ku­fan­ya hivyo ni kupunguza matumizi ikiwemo mishahara yao.


Taarifa zinaeleza kuwa nyota hao ni pamoja na Donny van de Beek, Jesse Lingard, Phil Jones, Eric Bailly, Anthony Martial, Diogo Dalot na Alex Telles ndiyo watawekwa sokoni.


Imeelezwa kuwa, nyota hao saba kuna baadhi watauzwa na wengine watapelekwa kwa mkopo katika timu nyingine kupata uzoefu zaidi.


Taarifa zinaeleza wakati hao wakitolewa kiungo wa timu hiyo, Paul Pogba ambaye mkataba wake unamalizika yeye atakuwa anaendelea na mazungumzo na timu hiyo kwa ajili ya dili jipya.


Jesse Lingard ni mchezaji ambaye yupo kwenye orodha ya wachezaji ambao wataondoka japo hivi karibuni kocha wake, Ole Gunnar Solskjaer amekuwa akieleza kuwa anamhitaji nyota huyo kwenye kikosi hicho.

Post a Comment

0 Comments