Recent-Post

NYOTA WAPYA MTIBWA SUGAR WAWEKA WAZI MALENGO YAO

BAADA ya kukamilisha usajili wao wa mkopo wa kujiunga na Mtibwa Sugar, Said Ndemla na Ibrahim Ame wametamba kuifanya klabu hiyo kuleta ushindani wa kweli katika Ligi Kuu Tanzania Bara kwa msimu ujao.

Said Ndema ambaye ni kiungo mshambuliaji na Ibrahim Ame ambaye ni beki wa kati wamejiunga na Mtibwa Sugar kwa mkopo wa msimu mzima.


Nyota hao wawili walikuwa wanakipiga ndani ya kikosi cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes.


Akizungumza na Championi Jumatatu, Ndemla alisema kuwa malengo yake kama mchezaji wa Mtibwa ni kuisaidia timu hiyo ili kuweza kufanya vizuri katika msimu ujao wa ligi na kufikia malengo ambayo wamejiwekea.


“Malengo yangu nikiwa kama mchezaji ni kuhakikisha kuwa naisaidia Mtibwa kuweza kufanya vizuri, nitapambana kwa ajili ya hilo nikishirikiana na wachezaji wenzangu na viongozi wa Mtibwa,”alisema Ndemla.


Naye Ibrahim Ame, alisema kuwa :“Kila kitu kipo sawa, kilichobaki ni kusubiri msimu uanze ili tupambane kwa ajili ya Mtibwa Sugar, malengo ni kufanya vizuri tofauti na misimu miwili iliyopita ambapo haikuwa mizuri kwa timu na sisi kama wachezaji tupo tayari kwa mapambano,”alisema beki huyo.

Post a Comment

0 Comments