Recent-Post

PELE YUPO FITI KWA SASA


 GWIJI wa zamani wa Brazil, Edson Arantes ulimwengu unamtambua kwa jina la Pele amesema kuwa kwa sasa anaendelea vizuri na afya yake ipo poa.

Pele alikuwa hospitalini kwa siku sita baada ya kufanyiwa upasuaji hivi karibuni kutokana na matatizo ya kiafya huku kinachomsumbua kikiwa ni siri na sasa anaendelea vizuri.

Mchezaji huyo wa zamani wa Brazil mwenye miaka 80 alikuwa anatajwa kuwa na hali mbaya hivi karibuni na taarifa zilikuwa zinadai kwamba alikuwa akizimia mara kwa mara.

Nyota huyo anatajwa kuwa ni mshambuliaji mkubwa wa muda wote anakumbukwa zama za kucheza soka la ushindani kwa kuwa alicheza jumla ya mechi 557 na kutupia mabao 538 katika ngazi ya klabu na kwenye timu yake ya taifa ya Brazil ni jumla ya mechi 92 na alitupia mabao 77.

Pele amesema:"Marafiki zangu nasema asanteni sana kwa jinsi ambavyo mmekuwa mkinitakia kila la heri. Namshukuru Mungu kwa kuwa ninaendelea vizuri na ninamshukuru kwa kunipa madakatri Dr.Fabio na Dr. Miguel kuangalia afya yangu," .

 

Post a Comment

0 Comments