Recent-Post

RAIS SAMIA AMETOA SHILINGI BILIONI 60 KWA AJILI YA WAKULIMA WA KOROSHO NCHINI- KATIBU MKUU CCM

 Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi  (CCM) Ndg. Daniel Chongolo amewahakikishia wakulima wa zao la korosho kutokatwa fedha za pembejeo sababu tayari serikali imetoa Bilioni 60 kwaajili ya pembejeo.


Kauli hiyo ameitoa jana tarehe 17 Septemba, 2021 mkoani Mtwara katika eneo la mnazi mmoja ikiwa ni muendelezo wa ziara ya Sekretarieti ya CCM Taifa  katika Mikoa ya Lindi, Mtwara, Ruvuma na Njombe.

Katibu Mkuu amefafanua kuwa, Miaka ya nyuma serikali ilikuwa ikitoa bilioni 50 kila msimu  ambapo wakulima walikuwa wakikatwa fedha hizo pindi wanapoenda kuuza Korosho zao.

Amesema, Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ametoa fedha hizo shilingi bilioni 60 kwa ajili ya pembejeo mwanzo wa msimu ili kuwasaidia wakulima kupata faida kubwa, na hakuna mkulima atakayekatwa fedha hizo kama ilivyokuwa awali.

Wakati huo huo, Katibu Mkuu ameeleza kuwa, Mwaka huu Rais Samia ameelekeza Korosho zote kupakiwa katika bandari ya Mtwara na sio ya Dar es Salaam kwaajili ya kusafirishwa, kwani bandari hiyo imegharimu shilingi Bilioni 100 kwa ajili ya upanuzi ili kuiongozea uwezo na kuwanufaisha wakulima wa mikoa ya kusini.


Post a Comment

0 Comments