Ratiba Ligi Kuu Tanzania Bara yaibua jambo

Wakati Ligi Kuu Bara ikitarajia kuanza takriban wiki tatu zijazo, kuchelewa kutoka kwa ratiba kumeibua jambo, ambapo wadau wa soka wamedai hatua hiyo inaathiri mchezo huo ndani na nje ya uwanja.

Ligi Kuu inatarajia kuanza Septemba 29, lakini hadi sasa ratiba haijatolewa, na wakizungumza kwa nyakati tofauti wadau wamesema maandalizi ya klabu yanakosa mbinu za kukabiliana na wapinzani wao katika mechi za mwanzo ambazo hutoa dira kwa timu kwa msimu husika wa soka.

Ofisa mtendaji mkuu wa zamani wa Azam FC, Saady Kawemba aliliambia Mwananchi jana kwamba, kutotoka mapema kwa ratiba kunaathari mabenchi ya ufundi kuandaa mbinu za kiunfundi kwa ajili ya mechi tano za kwanza kutokana kutojua wanakutana na timu zipi na aina ya michezo zinayocheza.


Hii inatokana na (Tanzania) kutojiandaa mapema kwenye kuingiza timu nne kwenye mashindano ya kimataifa, lakini pia kuchelewa kumalizika kwa ligi msimu uliopita,” alisema.

Athari ya nje ya uwanja ni kwenye kuandaa bajeti. Timu zitashindwa kuandaa bajeti zao kulingana na ratiba, lakini kama ingetoka mapema, basi viongozi wangejiandaa.”

Mchezaji wa zamani wa Yanga na mchambuzi wa soka, Ally Mayay alisema ratiba msimu huu ilishaonekana itakuwa ngumu kutokana na kuchelewa kumalizika kwa ligi msimu uliopita.

Kocha mkuu wa Namungo, Hemed Suleiman ‘Morocco’ alisema anaendelea na maandalizi suala la kuchelewa au kuwahi kutolewa kwa ratiba hawatoi nafasi ya kuwavuruga japo kikanuni sio vizuri.

“Kikubwa tunafahamu ligi inaanza siku gani, haituumizi vichwa japo kuna umuhimu wa kumfahamu mpinzani mapema,” alisema Morocco.

Katibu Mkuu wa Biashara United, Haji Mtete alisema: “Ratiba kuwahi inasaidia timu kujiandaa vizuri na kama mchezo wa kwanza ni wa kutoka na sio kuanzia nyumbani bajeti zinatakiwa kutengwa mapema.”

Wakati wadau wakihoji kwanini ratiba ya ligi inasuasua kutolewa, mtendaji mkuu wa Bodi ya Ligi, Almas Kasongo alisema leo wanatarajia kutangaza siku watakayoiachia ratiba hiyo kwa klabu.

Ndio nilisema ratiba inatoka wiki hii, lakini si ndio (wiki) imeanza , tutatoa nadhani kesho tunaweza kutoa ratiba au kutangaza siku ambayo tutaitoa hiyo ratiba,” alisema.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments