REKODI ZAIBEBA YANGA MBELE YA SIMBA

REKODI zinaibeba zaidi Yanga kuelekea mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba unaotarajiwa kuchezwa Septemba 25, mwaka huu kutokana na nyota yao kuwaka ndani ya mwaka 2021.

 

Timu hizo zikiwa zinakwenda kukutana Jumamosi hii kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar, tayari ndani ya mwaka huu zimekutana mara tatu katika michuano mitatu tofauti. Katika mechi hizo, Yanga imeibuka na ushindi mara mbili, huku Simba ikishinda mechi moja.

 

Ilikuwa Januari 13, 2021, katika fainali ya Kombe la Mapinduzi, visiwani Zanzibar, Simba walikutana na Yanga ambapo ushindi ulikuwa mikononi mwa Yanga ambayo ilishinda kwa penalti 4-3 baada ya muda wa kawaida matokeo kuwa 0-0.

 

Pia wakati Simba ikitamba na kikosi kipana cha gharama kubwa, Julai 3, mwaka huu walikutana Uwanja wa Mkapa, kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara, mwisho ubao ulisoma Simba 0-1 Yanga, huku bao likipachikwa na Zawadi Mauya.

 

Mchezo pekee ambao Yanga ilinyooshwa ndani ya 2021 walipokutana na Simba ulichezwa Julai 25, kwenye fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam iliyochezwa Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma, Simba ilishinda kwa bao 1-0 lililopachikwa na Taddeo Lwanga.


Maandalizi ya mchezo huo yapo tayari ambapo kila timu imeweka wazi kwamba inahitaji ushindi ili kusepa na Ngao ya Jamii.


Mchezo huo unatarajiwa kuanza majira ya saa 11:00 jioni.Licha ya rekodi kuibeba Yanga haina maana kwamba inaweza kushinda kwa wepesi ikiwa haitafanya maandalizi jambo la msingi ambalo litaamua mshindi ni dakika 90 uwanjani.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments