Recent-Post

RONALDO AANZA KAZI MAN UNITED, ATUPIA MBILI

 MSHAMBULIAJI mpya wa Manchester United ya Uingereza, Cristiano Ronaldo amenza kazi na Klabu hiyo na kufunga mabao mawili katika mchezo wa Ligi Kuu Soka nchini Uingereza (EPL) dhidi ya Newcastle United kwenye ushindi wa jumla wa bao 4-1 katika dimba la Old Trafford nchini humo.


Ronaldo kwa mara ya kwanza akivaa Uzi wa Manchester United na wakiwa nyumbani Ngome Kongwe, alifanikiwa kupata mabao hayo mawili kwa umahiri kabisa katika dakika ya 45+2’ na dakika ya 62’ ya mchezo huo huku mabao mengine yakifungwa na Mshambuliaji Bruno Fernandes dakika ya 80’ na Jesse Lingard dakika ya 90+2’ wakati bao la Newcastle likifungwa na J. Manquillo dakika ya 56’.

Msimu huu ni msimu mpya kwa Nyota Cristiano Ronaldo kucheza Man United baada ya awali, mwaka 2003 hadi 2009 wakati timu hiyo ikiwa chini ya Kocha Mkuu, Sir Alex Ferguson ambapo baadae CR7 alitimkia Real Madrid alipocheza kati ya mwaka 2009 hadi 2018 na alitua Italia katika timu ya Juventus na kucheza kati ya misimu ya 2018 hadi 2021.

Ni rasmi sasa Cristiano Ronaldo dos Santos Aveiro maarufu CR7 amerejea tena Manchester United chini ya Kocha Mkuu Ole Gunnar Solskjær.


 

Post a Comment

0 Comments