Recent-Post

Samatta afungua akaunti huko Europa

MSHAMBULIAJI wa Tanzania, Mbwana Samatta anayeichezea timu ya Royal Antwerp ya nchini Ubeligiji amefungua rasmi akaunti yake ya mabao jana.

Samatta amefungua akaunti hiyo jana usiku katika mchezo wa Europa dhidi ya Olympiacos huku wakipoteza 2-1 na yeye akiwa ndio mfungaji wa bao hilo pekee.

Mchezo huo ni wa kwanza kwa Royal Antwerp katika Europa League na wameanza kwa kupoteza wakiwa ugenini ambapo Samatta alifunga bao hilo dakika ya 74 kwa kichwa akimalizia krosi.

Samatta amejiunga na timu hiyo akitokea Fenerbahce ambapo alishindwa kutamba kiasi cha kumtoa kwa mkopo wenye kipengele cha kuuzwa moja kwa moja.

Post a Comment

0 Comments