Recent-Post

Serikali yawapa fursa wafanyabiashara kutangaza bidhaa zao nje ya nchi

Serikali imeweka mabanda ya maonesho nchini China, Kenya na Dubai kwa ajili ya Watanzania kupeleka bidhaa zao kama njia ya kutambulika na kuunganishwa na masoko mbalimbali duniani.

Hayo yameelezwa leo Septemba 19 na Msemaji mkuu wa Serikali Gerson Msigwa wakati akizungumza na waandishi wa habari katika taarifa yake ya wiki jijini hapa.

Amesema Serikali itagharamia ya kuweka mabanda katika nchi hizo, huku wajasiriamali na Watanzania wakibaki na jukumu la kwenda na bidhaa zao na kuweka kwenye mabanda ambayo Serikali imeyandaa.

Amesema licha ya mchango huo Serikali inawasimamia wazalishaji kuzitambulisha bidhaa kwa jina la nchi ili kwenda sambamba na kuboresha bidhaa hizo.

“Nitoe wito kwa Watanzania kuwa bidhaa zote zinazozalishwa nchini zitambulisheni kama zinatoka Tanzania. Pamoja na hayo yote, nchi yetu imekuwa ikifanya maonesho mbalimbali ambayo yanatambulisha bidhaa zetu tumekuwa na maonesho ya sabasaba na watanzania wanaoneshwa ni kwa namna gani ya kuunganishwa na masoko mbalimbali duniani,” amesema.

                By Mainda Mhando

Post a Comment

0 Comments