TIMU ya Simba rasmi itacheza na TP Mazembe ya DR Congo katika kilele cha siku ya Simba Day Septemba 19, Jijini Dar es Salaam.
Sababu kubwa iliyotajwa ya kuichagua TP Mazembe ni kwa sababu ni miongoni mwa timu kubwa Barani Afrika na mabingwa mara tano wa Ligi ya Mabingwa Afrika hivyo italeta ushindani katika kikosi hicho ambacho kimekuwa na maingizo mapya.
Mara ya mwisho kwa timu hizo kukutana ilikuwa Februari 2 Mwaka huu kwenye kombe la Simba maarufu kama (Simba super Cup) ambapo mechi iliisha kwa sare ya 0-0.
Kikosi cha Simba kwa sasa kipo jijini Arusha kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya baada ya kumaliza kambi ya wiki mbili nchini Morocco.
By Daudi Elibahati
0 Comments