Simba: Manara tutamjibu kwa vitendo

            

MASHABIKI wa Simba mkoa wa Mbeya wamesema licha ya kuondokewa na nyota wao wawili, Luis Miquissone na Clatous Chama, bado timu hiyo itazidi kutesa kwenye Ligi Kuu Bara, huku wakitupa kijembe kwa aliyekuwa Afisa habari wao, Haji Manara.

Miquissone amesajliwa na klabu ya Al Ahly ya Misri, wakati Chama ametimkia katika timu ya RS Berkane ya Morocco.

Mbali na nyota hao pia aliyekuwa Afisa habari wa timu hiyo, Haji Manara naye hatakuwa na mabingwa hao watetezi baada ya hivi karibuni kutangazwa kuwa msemaji wa Yanga na kuzua mjadala kila kona.

Mwenyekiti wa Simba Mkoa wa Mbeya, Abel Edson alisema mashabiki wasiwe na wasiwasi kwani uongozi umefanya usajili bora wa mbadala wa nyota hao hivyo msimu ujao kazi iendelee.

Alisema kwa sasa hawawezi kujibizana kwa maneno dhidi ya Manara na badala yake watajibu kwa vitendo kwa kufanya kweli katika Ligi Kuu na Ligi ya Mabingwa Afrika.

Niwaombe mashabiki wenzangu tusijibizane na huyo msaliti, tuwaunge mkono viongozi wetu kwani kazi wanayoifanya ni kubwa na pengo la Miquisone na Chama litazibika,” alisema Edson.

Naye Fausta Elias mwenyekiti wa Simba tawi la Unyamwanga alisema matarajio yao msimu ujao ni kuendelea kutawala soka la hapa nchini,lakini hata nje watawakilisha vyema.

Kimsingi ni kuwa wamoja kwa kipindi hiki kama ambavyo tumefanya msimu uliopita, tuwasapoti na kuwapa ushirikiano wachezaji wetu pamoja na uongozi wa juu ili tuendelea kufanya vizuri kwenye mashindano yote msimu ujaio,” alisema Fausta.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments