Recent-Post

Taifa Stars kileleni

USHINDI wa 3-2 waliopata Tanzania dhidi ya Madagascar unaifanya waongoze kundi J wakiwa na pointi nne mpaka sasa.

Stars inaongoza kundi hilo kwa tofauti ya mabao mawili wakiwa na jumla ya mabao manne huku Benin wanaoshika nafasi ya pili wakiwa na mabao mawili na pointi nne.

Katika kundi hilo nafasi ya tatu inashikiliwa na DR Congo wenye pointi mbili huku nafasi ya mwisho ikishikiliwa na Madagascar wasiokuwa na pointi.

Kwenye mchezo wa Stars dhidi ya Madagascar Stats walionyesha kuhitaji mabao ya mapema zaidi na waliweza kupata lakini kwene kujilinda walionekana kulizika.

Dakika ya kwanza Stars ilipata bao kupitia mkwaju wa penalti baada ya Saimon Msuva kufanyiwa madhambi  ndani ya boki na kipa wa Madagascar, na Erasto Nyoni aliweka mpira wavuni.

Stars waliendelea kuliandama lango la Madagascar lakini umakini kwenye kumalizia walionekana kutotumia nafasi walizokuwa wanapata.

full pic 3

Dakika 20 Reliants Lusajo  wa Stars alipiga krosi na kuonganishwa kwa kichwa na Mbwana Samatta mpira ukatoka nje kidogo ya goli.

Dakika 25  Stars ilipata bao la pili kupitia kwa kiungo Novatus Dismas aliyepiga shuti la chini chini na mpira kwenda wavuni.

Madagascar walifanya mabadiliko dakika 29 akitoka Manampisoa Lalaina na kuingia Rakotomalilala Njiva.

full pic 2

Dakika 33 mshambuliaji wa Stars, Mbwana Samatta alionyeshewa kadi ya njano baada ya kuonekana akikaa na mpira bila sababu ulipokuwa umetoka.

Mabadiliko ya kuingia   Njiva yalijibu dakika 35 baada ya kuifungia bao kwenye mchezo huo na kuanza kuwarejesha mchezoni.

Baada ya bao hilo Madagascar walianza kubadilika na kutulia wakifanya mashambulizi ya pole pole kwenda langoni kww Stars.

Beki Erasto Nyoni wa Stars  dakika 44 alimfanyia madhambi mshambuliaji wa Madagascar, Abdallah Hakim na kuonyeshewa kadi ya njano.

Madhambi hayo yaliwafanya Madagascar wapate bao kupitia faulo iliyopigwa na Fontaine Thomas aliyepiga mpira na kwenda moja kwa moja wavuni.
Madagascar kwenye kipindi cha pili walianza kwa kushambulia lakini mabeki wa Stars wakiongozwa na Bakari Mwamnyeto waliwatuliza.

Stars walikuwa wakitumia upande wa mawinga ambao walikuwa wanacheza Mbwana Samatta na Simon Msuva.

Dakika 52 Stars ilipata bao la tatu kupitia kwa Feisal Salum ambaye alipokea pasi kutoka kwa Mbwana Samatta na yeye aliutuliza na kupiga shuti la chinichini na mpira kwenda wavuni.

full pic 1

Dakika 64 Madagascar waliingia  Voax Paulin na  Amada Samuel  na kutoka  Hery Charles na Lassoin Poic wakati huo Stars walitoka Novatus Disma na Reliants Lusajo nafasi zao zikichukuliwa na Nickson Kibabage na Mudathir Yahya.

Madagascar walionyesha kuhitaji bao la kusawazisha baada ya kufanya mabadiliko dakika 76 wakiingia Carlos na Ramalingon Alexandre wakitoka  Mombris Jerome na  Anicet wakati huo huo Tanzania alitoka   Feisal Salum na kuingia Salum Abubakari.

full pic 4

Stars ilitaka kupata bao la nne dakika 80 baada ya Salum Abubakar kumpigia pasi Mbwana Samatta ambaye alitulia na kupiga pasi kwa Simon Msuva aliyeingia ndani ya boksi na kupiga shuti lililotoka nje kidogo ya goli.

Post a Comment

0 Comments