Utata waibuka alipo mtuhumiwa kesi ya kina Mbowe

Utata umeibuka alipo mmoja wa watuhumiwa katika kesi ya kufadhili ugaidi inayomhusisha Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake, aitwaye Moses Lijenge kama yuko hai au amefariki dunia.

Utata huo umeibuliwa leo Jumanne Septemba 28, 2021 na shahidi wa pili wa utetezi katika kesi ndogo ndani ya kesi ya msingi, Mohamed Ling'wenya wakati akihojiwa na mawakili .

Shahidi huyo ambaye ni mshtakiwa wa tatu katika kesi hiyo anatoa ushahidi kwa lengo la kujiridhisha uhalali wa utoaji wa maelezo ya mshtakiwa wa pili, Adamu Kasekwa ambayo mawakili wa utetezi walipinga yasipokewe mahakamani kama kielelezo cha ushahidi upande wa mashtaka wakidai yalichukuliwa nje ya muda wa kisheria na mshtakiwa huyo alitoa maelezo hayo baada ya kuteswa na kutishiwa.

Soma zaidi: Shahidi kesi ya Mbowe aeleza alivyoshinda njaa siku kumi polisi

Awali, shahidi wa kwanza katika kesi ya msingi, Kamanda wa Polisi Mkoa  wa Kinondoni, Ramadhani Kingai aliieleza mahakama kuwa wakati wakiwakamata watuhumiwa wawili huko Moshi, mtuhumiwa wa tatu Lijenge hawakumpat,  licha ya kumtafuta sehemu mbalimbali, hivyo wakaamua kuwapeleka Dar es Salaam watuhumiwa hao wawili.

Lakini katika ushahidi wake wa msingi jana, shahidi huyo alidai wakati wakitolewa kituo cha polisi kwenda Mbweni mmoja wa maaskari alimweleza kuwa mwenzake Moses Lijenge wameshamtupa kwa sababu alijidai kuwakimbia.

Alipohojiwa na wakili wa Mbowe, Peter Kibagala leo Jumanne shahidi huyo amedai alivyoelezwa na askari yule kuwa mwenzao Lijenge wameshamtupa alielewa kuwa ameshauawa.

Soma zaidi: Shahidi wa tatu kesi ndogo ya Mbowe, wenzake aanza kutoa ushahidi

Akihojiwa zaidi na Kibatala, Mohamed amedai hajawahi kumsikia akitajwa mahali popote na upande wa mashtaka kama Lijenge ataunganishwa katika kesi hiyo, hivyo hajui kwa hakika kama yuko hai au ameshafariki.

Kwa sasa shahidi huyo wa pili upande wa utetezi katika kesi ndogo anaendelea kuhojiwa na upande wa mashtaka kuhusiana na ushahidi wake.

Soma zaidi: Boaz, Kingai kizimbani kesi ya Mbowe

Mbali na Mbowe, Mohamed na Adamu mshtakiwa mwingine katika kesi hiyo ni Halfani Hassan.

Wote wanakabiliwa na mashtaka sita ya  ugaidi, wakidaiwa kuyatenda kwa nyakati tofauti Agosti 2020.

By James Magai

 

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments