Staa Vanessa Mdee na mchumba wake, Rotimi kupitia mitandao ya kijamii wa Instagram wameposti ujumbe unaoshiria kuwa wanatarajia kupata kupata mtoto wa kiume hivi karibuni.
Hayo yamebainika leo Jumanne Septemba 7, 2021 kupitia kurasa zao ambapo kwa nyakati tofauti waliposti picha mbalimbali zikimwonyesha Vanessa kuwa mjamzito.
Mahusiano ya wawili waliyaweka wazi mwaka 2019 ikiwa ni miezi michache tangu alipoachana na aliyekuwa mpenzi wake wa muda mrefu, msanii wa Bongo fleva, Juma Jux.
Wawili hawa waliamua kuyaweka wazi mahusiano yao mwaka 2019 na Desemba 2020, Rotimi ambaye ni mwanamuziki na muigizaji mwenye makazi yake nchini Marekani, alimvalisha pete mrembo huyo.
Licha ya nyakati tofauti kuwepo kwa tetesi za kuwa mjamzito, Vanessa alikanusha hilo na kuwalaumu waliokuwa wanasema hilo kuwa wamesababisha mama yake kupaniki.
Rotimi ameandika "Zawadi kubwa imekuwa ni wewe, umebadilisha maisha yangu na sasa tumeungana milele kumlea mtoto wetu,"
Soma hapa: Vanessa Mdee avishwa pete ya uchumba
Naomba mtoto wetu awe na moyo wako, akili, na imani yako, ninaahidi kukulinda wewe na mtoto wetu kwa kila nilichonacho,” ameeleza
Kwa upande wake Vanessa ameandika "Zawadi kubwa kuliko, asante Yesu kwa kutuchagua, kutuheshimisha…tuna furaha sana,” ameandika Vanessa.
0 Comments