Watuhumiwa wawili waliotoroka mahabusu wakamatwa

 


Kaimu kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Daniel Shila amefunguka na kusema mahabusu waliotoroka katika kituo cha Polisi cha Maturubai, Mbagala jijini hapa ni 16 na kati ya hao wawili wameshakamatwa.

Awali taarifa zilizopatikana kutoka kwa mmoja wa askari wa kituo hicho, zilieleza kuwepo kwa watuhumiwa zaidi ya 20 waliotoroka katika kituo hicho, baada ya kumpiga askari na kisha kuvunja lango la chumba cha mahabusu na kukimbia.  

Akizungumza na Mwananchi leo kwa simu leo Septemba 6, Kaimu kamanda huyo ambaye ni Mkuu wa Upelelezi wa Kanda hiyo, Shila amesema mahabusu  waliokuwa ndani ya  ya kituo hicho walikuwa 81 kati ya hao 16 walitoroka na wawili walikamatwa.

Soma hapa:Mahabusu 20 watoroka kituo cha polisi

Amesema watuhumiwa hao waliokamatwa walikuwa na makosa madogomadogo yanayotokana na polisi ikiwemo bangi na gongo.


Watuhumiwa wawili tuliwakamata jana hadi na sasa polisi wamesambaa sehemu mbalimbali kwa ajili ya kuwatafuta na vilevile wale wahalifu hawana madhara kwa jamii kwa kuwa wengi wao waliotoroka walikamatwa na polisi walipokuwa wanafanya doria," amesema na kuongeza.

Walikuwa kwenye ukaguzi lazima ufungue lango la mahabusu ili waingie ndani kwa kuwa walikuwa wengi walisukuma mlango na mahabusu hao walitoka nje."

Tukio hilo la aina yake lilitokea juzi kuanzia saa moja usiku katika kituo hicho cha wilaya ya kipolisi ya Mbagala wilayani Temeke, mkoani Dar es Salaam.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments