Waziri Ummy - Fanyeni Msawazo Wa Waalimu Nchini Waziri Ummy

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Ummy Mwalimu ameielekeza Tume ya Utumishi wa waalimu nchini  kuhakikisha wanafanya msawazo wa waalinu katika Mamlaka za Serikali za Mitaa  ili kuweka uwiano sawa wa waalimu nchini.

Akiongea na Menejimenti ya Tume ya Utumishi wa waalimu Jijini Dodoma Waziri Ummy amaesema kumekuwepo na changamoto kubwa kwa baadhi ya shule kuwa na waalimu wengi huku nyingine zikikosa waalimu, hivyo  ni wajibu wa tume kuhakikisha suala hilo linashughulikiwa kwa wakati

Waziri Ummy amesema kuna baadhi ya shule zina watoto wengi lakini waalimu ni wachache huku shule nyingine zikiwa na waalimu wengi wanafunzi wachache, ni vyema kukawa na uwiano ulio sawa katika shule zote nchini.

Tunafahamu kuwa zipo shule ambazo zinawaalimu wachache hasa maeneo ya vijijini, lakini nyingine zinawaalimu wengi, suala hili halikubaliki, suala hili linahitajika kufanyiwa kazi ingawa mara nyingi serikali inaangalia idadi ya wanafunzi “amesisitiza Waziri Ummy

Waziri Ummy ameendelea kueleza kuwa kutokufanya msawazo hatuwatendei haki wanafunzi walioko vijijini hasa katika maeneo ya pembezoni ni wajibu wa tume kuhakikisha shule zote zinakuwa na idadi sawa ya waalimu

Aidha amewaelekeza Tume ya Utumishi wa Waalimu nchini kutumia mifumo ya kielektroniki katika kutatua kero za waalimu nchini ili kupunguza changamoto hizo kwa haraka na kutoa mrejesho kwa waalimu kwa wakati



 
                                              Na. Angela Msimbira TAMISEMI

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments