Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari nchini Tanzania, Dk Ashatu Kijaji
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari nchini Tanzania, Dk Ashatu Kijaji amesema hatakuwa na uvumilivu kwa wanahabari watakaojihusisha na habari zinazolichafua Taifa.
Hii ni mara ya kwanza kwa Dk Kijaji kuzungumza na umma baada ya kuteuliwa na kuapishwa Septemba 13 2021.
Dk Kijaji ameyasema hayo leo Alhamis Septemba 16 2021 wakati akizindua kamati ya ukaguzi ya Tehema.
Waziri huyo ametaka kupunguzwa kwa malalamiko yanayohusiana na idara ya Habari waliongezewa katika wizara hiyo Septemba 12 2021.
“Wanahabari lazima tuelewane hapa lazima tuchuje nini watanzania wanataka kukisikia, kile unachokiandika, kile unachokitangaza kiwe na maslahi mapana,” amesema.
Amesema kwa kila mmoja kujivunia kuwa Mtanzania kutasaidia katika kuepusha vishawishi vya kulichafua Taifa.
Amesema pia kutaepusha vishawishi vya kuwafanya watanzania wasikie wasichotarajia kukisikia.
“Na kwa hili niseme sitokuwa na uvumilivu tutasimamia maadili na kamati tuwezesheni ili Taifa lipate taarifa zinazohitajika tu na zisizohitajika hazuzitaki,” amesema.
Dodoma.
0 Comments