Recent-Post

YANGA BINGWA NGAO YA JAMII MSIMU WA 2021/22


Dakika 90 za Mchezo dhidi ya Simba na Yanga zimemalizika jiono hii katika Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es salaam kwa Yanga SC kuichapa Simba SC Bao 1- 0.

Yanga ilipata bao dakika 13 ya mchezo kupitia kwa mshambuliaji wake Fiston Mayele kupiga shuti kali lililomshinda mlinda mlango wa Simba Aishi Manula.

Bao hilo pekee la mshambuliaji Mkongo, Fiston Kalala Mayele limetosha kuipa Yanga SC ushindi wa 1-0 katika mechi hiyo ya Ngao ya Jamii.

Simba SC, washindi wa Ngao kwa misimu minne mfululizo iliyopita walimaliza pungufu baada ya kiungo wao Mganda, Thadeo Lwanga kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 90 kufuatia kuonyeshwa kadi ya pili ya njano kwa kumchezea rafu kiungo Mzanzibari wa Yanga, Feisal Salum.

Post a Comment

0 Comments