Recent-Post

Yanga fasta yaandaa mbadala


Yanga inamwandaa Mukoko Tomombe ambaye baada ya Yanga kufungwa na Zanaco alizuia safari ya kwenda timu ya taifa ili azibe nafasi ya Aucho.

Nafasi ya Mayele aliyefunga mara mbili ndani ya siku 7 katika mechi za kirafiki, kazi yake amekabidhiwa Heritier Makambo huku pia Yacouba Sogne na Yusuf Athuman nao wakipewa makali.

Eneo la Djuma ambaye mashabiki wa Yanga wanaonekana kumuelewa, Kibwana Shomari yuko tayari kufanya kazi hiyo kama ilivyokuwa msimu uliopita. Kazi hiyo ya kuwapika mastaa hao imeanza jana asubuhi na kuwafanya mabosi wa Yanga kushusha presha huku wakiendelea kuwapigania mastaa hao.

                                Dar es Salaam


Post a Comment

0 Comments