Recent-Post

YANGA WATUA NIGERIA,MATIZI KUPIGA LEO

WAWAKILISHI wa Tanzania katika Ligi ya Mabingwa Afrika,  Yanga leo Septemba 18 wamewasili salama nchini Nigeria.

Jana Septemba 17 kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi kilianza safari kuwafuata wapinzani wao Rivers United. 

Mchezo huo unaotarajiwa kuchezwa Septemba 19, nchini Nigeria ni wa marudio baada ya ule wa awali uliochezwa Uwanja wa Mkapa ubao kusoma Yanga 0-1 Rivers United. 


Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Yanga, Haji Manara amesema kuwa wapo salama na tayari kwa ajili ya mchezo huo ambao utakuwa ni mgumu kwa timu zote mbili.

Tumefika salama Nigeri na tuna msafara wa maana ikiwa ni pamoja na viongozi na mashabiki ambao wapo bega kwa bega na timu, kikubwa ni kuona tunapata ushindi.

Wengi walikuwa wanapenda kusafiri na timu ila kutokana  na sababu mbalimbali wameshindwa na hawa waliopo watawakilisha wengine.

Leo timu itafanya mazoezi ya mwisho kwa ajili ya mchezo ujao na tukimaliza tu mchezo ndege yetu tuliyokodi kutoka shirika la ndegea Tanzania itaturudisha," amesema.

Yanga inakibarua cha kusaka ushindi wa mabao zaidi ya mawili na kazi nyingine ni kulinda lango lao lisiruhusu bao jingine la kufungwa ili kusonga mbele.

Post a Comment

0 Comments