YANGA YAPOTEZA KWA MKAPA MBELE YA RIVERS UNITED


WAWAKILISHI wa Tanzania, Yanga kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika leo wameanza kwa kupoteza mchezo wa awali hatua ya Ligi ya Mabingwa wakiwa Uwanja wa Mkapa.

Mchezo wa leo ulikuwa na ushindani mkubwa ambapo Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi ilikuwa inapewa nafasi kubwa ya kuibuka na ushindi kwa kuwa ilikuwa ipo nyumbani ila ghafla mambo yalikuwa ni mazito.

Dakika 45 zilikamilika kwa timu zote kutoshana nguvu jambo ambalo liliwafanya waende kenye vyumba vya kubadilisha nguo ubao wa Uwanja wa Mkapa ukisoma Yanga 0-0 Rivers United .

Kipindi cha pili ngoma ilipinduka baada ya Rivers United kuongeza kasi ya mashambulizi na kupata kona ya kwanza dakika ya 50 iliyoleta bao lililopachikwa na nyota wao Moses Omdumuke .

Ilikuwa ni kichwa kilichomshinda kipa namba moja Diarra na kuwafanya Rivers United kusepa na ushindi.


Jitihada za Yanga kupitia kwa mshambuliaji wao Heritier Makambo ambaye alimpisha Ditram Nchimbi hazikuweza kuleta matunda na kuwafanya wapoteze furaha katika mchezo wa kwanza.

Yanga ina kazi ya kwenda kusaka ushindi nchini Nigeria kwenye mchezo wa marudio wa Ligi ya Mabingwa unaotarajiwa kuchezwa Septemba 18.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments