Recent-Post

YANGA YASIMULIA FITINA WALIZOFANYIWA NIGERIA

UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kuwa walifanyiwa mbinu mbaya ili kuwatoa mchezoni na wapinzani wa Rivers United katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika nchini Nigeria.

Mkuu wa Kitengo cha Masuala ya Mawasiliano ndani ya Yanga, Hassan Bumbuli ameweka wazi kuwa walifanyiwa mambo ambayo sio ya kiuungwana ikiwa ni mbinu ya wapinzani wao.
 
Tunamshukuru Mungu tumemaliza mchezo wetu salama na tulipata nafasi kama tatu hivi ambazo zilikuwa ni penalti za wazi ila mwamuzi akapeta nazo.

Wenzetu walikuja na ajenda ambapo wachezaji wanne wa kikosi cha kwanza walikuwa wanatajwa kuwa wana COVID 19 lakini wameshindwa kuthibitisha hilo.

Tunashukuru kwa ajili ya wachezaji wetu ambao waliweza kupambana kwa ajili ya timu na mwisho wa siku tumeshindwa kupata kile ambacho tulikuwa tunatarajia.

Tumepata somo kubwa katika hili hasa kwenye upande wa COVID 19. Tunarudi kujipanga kwa ajili ya mashindano mengine, mashabiki wasiwe wanyonge bado tupo imara na tuna kikosi kizuri," amesema Bumbuli.

Wachezaji ambao walikuwa wanatajwa kuwa na COVID 19 ni Yacouba Songne, Mukoko Tonombe, Feisal Salum pamoja na kipa Diarra ila mwisho wa siku wote waliweza kucheza mchezo huo jana.

Nchini Nigeria Yanga ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0 na kufanya itolewe kwenye Ligi ya Mabingwa kwa jumla ya mabao 2-0 kwa sababu kwenye mchezo wa awali uliochezwa Uwanja wa Mkapa, Yanga ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0.

Tayari kikosi cha Yanga kimerejea Dar leo Septemba 20 kwa ajili ya maandalizi ya msimu wa 2021/22 kazi yao inayofuata ni Septemba 25 itakuwa dhidi ya Simba, mchezo wa Ngao ya Jamii.

Post a Comment

0 Comments