Recent-Post

Bananga arejea CCM

Aliyekuwa Diwani wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) katika Kata ya Sombetini Jiji la Arusha, Ally Bananga amerejea Chama Cha Mapinduzi (CCM).


Bananga ametangaza leo Jumapili Oktoba 17, 2021 katika mkutano wa hadhara wa Rais Samia Suluhu uliofanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid.


Akizungumza katika mkutano huo, Bangana ambaye alikuwa mwanachama machachari akiwa katika timu ya kampeni ya aliyekuwa mgombea Urais wa Chadema Tundu Lissu amesema amerejea CCM kumuunga mkono Rais Samia.


Bananga ambaye alikuwa Diwani kwa miaka sita, ameeleza pia kuirudishwa na uamuzi wa Serikali kutoa fedha za ujenzi wa hospitali ya Jiji la Arusha ambayo alikuwa mmoja wa madiwani waliopitisha mradi huo.

Bananga amesema ameridhishwa na utendaji wa Rais Samia na anaimani atakwenda peponi na atakutana naye.
"Najua na Mimi ntafika peponi ila nikiingia nisipokukuta nitatoka" amesema


Baada ya kutangaza uamuzi huo, Rais Samia alimshuru Benanga kwa zawadi aliyompa kwa kurejea CCM.
Rais Samia amesema yale aliyokuwa anayapigania akiwa kule atamrejeshea ayafanyie kazi.

Post a Comment

0 Comments