BIASHARA UNITED HALI NI TETE,HAKUNA TIKETI ZA KIMATAIFA

 


UONGOZI wa Biashara United umeweka wazi kuwa kwa sasa vichwa vinawauma kuhusu suala la usafiri wa wachezaji wao kuelekea nchini Libya kwa ajili ya mchezo wa kimataifa wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Al Ahly Tripoli.

Biashara United ina kibarua cha kusaka ushindi katika mchezo wa Kombe la Shirikisho raundi ya kwanza dhidi ya Al Ahly Tripoli ya Libya ambao unatarajiwa kuchezwa Oktoba 15, Uwanja wa Mkapa.

Seleman Mataso, Mwenyekiti wa Biashara United amesema kuwa kuhusu mchezo wao wa nyumbani hawana tatizo ila kinachowaumiza ni ule wa marudio nchini Libya hali ni mbaya.

Akizungumza na Saleh Jembe, Mataso alibainisha kuwa wanahitaji kufanya vizuri kimataifa ila hali ni tete kwenye upande wa mkwanja.

“Hali ni mbaya sana kwa ajili ya mchezo wetu wa marudio ugenini, kwa muda huu gharama za matumizi ya safari mambo hayajakaa sawa na hata tiketi pia bado hatujapata hivyo wadau watupe sapoti katika hili,” .

Biashara United inayonolewa na Kocha Mkuu Patrick Odhhiambo iliweza kufika katika hatua hiyo baada ya ushindi mbele ya Dikhil.Mchezo wa marudio unatarajiwa kuchezwa Oktoba 23 nchini Libya.

 Imeandikwa na Dizo_Click

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments