Recent-Post

DITOPILE AELEZA SIFA ZA MGOMBEA UBUNGE WA CCM JIMBO LA USHETU

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Dodoma, Mariam Ditopile leo amejumuika na wanaCCM wenzake katika Kata ya Bulungwa kumuombea kura Mgombea Ubunge wa CCM Jimbo la Ushetu Mkoani Shinyanga, Emmanuel Cherehani huku akiwataka watanzania kutega sikio siku ya Jumapili kumsikiliza Rais Samia Suluhu Hassan.

Akizungumza na wananchi wa Kata hiyo, Ditopile amesema Cherehani ambaye alipitishwa na Chama Cha Mapinduzi kuwa mgombea Ubunge wa Ushetu anatosha na ana sifa zote za kuwa muakilishi wao bungeni.

Jumapili Mama Samia ana jambo Kubwa na Zito kweli kweli nawaomba wana Ushetu na watanzania kwa ujumla Nchi nzima Mtege Sikio, Mama huyu yupo kazini anahangaika na shida za watanzania, tukae kwenye redio, na TV tumskilize, na tukitoka tukawasimulie wengine.

Tunaye Rais mahiri na shupavu na nyie mmeona anafaa mmempa Uchifu leo kwenye historia ya nchi yetu pamoja na kwamba tuna Rais wa kwanza mwanamke tuna Chifu Mwanamke Chifu Hangaya Samia Nyota inayong’aa "
Mbunge Mariam Ditopile, Ufungaji Kampeni Jimbo la Ushetu,

Nawaomba wana Ushetu watuletee Cherehani kule bungeni nimelelewa na wasukuma najua ukarimu wenu, nitashirikiana naye kule Bungeni hatokuwa mgeni atawapambania kuwaletea maendeleo"
Amesema Ditopile Akimuombea Kura Mgombea Ubunge Kwa Tiketi Ya Ccm Jimbo la Ushetu Leo.

Jimbo la Ushetu limeingia kwenye Uchaguzi mdogo kufuatia kifo cha Mbunge wa Jimbo hilo na aliyekua Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Elias Kuandikwa.

Picha Na Dix Uvccm Taifa.
Picha Na Dix uvccm Taifa.

Post a Comment

0 Comments