HIKI HAPA KIKOSI CHA KWANZA YANGA NA DAKIKA ZA MASTAA


BAADA ya kucheza mechi mbili, kituo kinachofuata kwa Yanga ni Oktoba 19 dhidi ya KMC mchezo unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Majimaji, Songea.

Huo utakuwa ni mchezo wa mzunguko wa tatu na wa tatu kwa Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi raia wa Tunisia kukaa kwenye benchi kwa msimu wa 2021/22.

Mechi zote mbili ambazo ameongoza za ligi wameshinda ilikuwa mbele ya Kagera Sugar na ule wa pili dhidi ya Geita Gold.

 Tayari Nabi kuna wachezaji ambao wanaonekana kupenya jumla kikosi cha kwanza na kwenye mechi mbili za ligi mbele ya Kagera Sugar, Uwanja wa Kaitaba na ule dhidi ya Geita Gold, Uwanja wa Mkapa nyota hao walianza kikosi cha kwanza.

 Kwenye mechi mbili Nabi hakubadilisha  hata mchezaji mmoja kutoka wale ambao alianza nao mbele ya Kagera Sugar kwa kuwa aliendelea nao pia katika mchezo wake wa pili dhidi ya Geita Gold.

Hizi hapa dakika za mastaa wa Nabi ndani ya Yanga:-Djigui Diarra dakika 180, Kibwana Shomari dakika 180,Djuma Shaban dakika 180.


Dickson Job dakika 180,Yanick Bangala  dakika 180,Khalid Aucho dakika 180,Jesus Moloko dakika 122 na ametupia pia bao moja, Yacouba Songne dakika 143 yeye ana pasi moja ya bao, Feisal Salum dakika 167 huyu ametupa bao moja na alikuwa mchezaji wa kwanza kufunga msimu wa 2021/22, Fiston Mayele ametumia dakika 152.


Kwa upande wa wachezaji wake wa akiba ni Heritier Makambo alimpa jumla ya dakika 54, Deus Kaseke dakika 58 na Rajab Athuman dakika 9.

Post a Comment

0 Comments