MABOSI SIMBA WATANGULIA BOTSWANA,WAKWEPA HUJUMA, KAZI INAENDELEA

 


 KATIKA kuhakikisha wanakwepa hujuma za wapinzani wao Jwaneng Galaxy ya nchini Botswana, viongozi wa Simba wameshtuka na haraka wakabadili uwanja.


Timu hizo zinatarajiwa kuvaana Jumapili hii na Simba ndiyo mgeni katika mchezo huo utakaopigwa Botswana.


Simba tayari imewatanguliza viongozi watatu nchini huko kwa ajili ya kuandaa mazingira ambao ni Mratibu Ali Abbas, mpishi wao Mkuu Samweli Mtundu ‘Sam’ na Mtaalamu wa tathmini, Culvin Mavhunga.


Timu hiyo hivi sasa ipo kambini ikiendelea kujifua kwenye Uwanja wa Boko Beach jijini Dar es Salaam.


Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Championi Jumatatu, baada ya viongozi wa timu hiyo kutua nchini huko, haraka walibadili uwanja wa kuwafanyia mazoezi waliopanga kuutumia awali.


Mtoa taarifa huyo alisema kuwa sababu ya kubadili ya uwanja huo ni kukwepa hujuma baada ya kushtukia baadhi ya vitu kutoka kwa wapinzani wao.


Aliongeza kuwa viongozi hao wamepata uwanja mwingine watakaoutumia kwa ajili ya mazoezi kwa muda wa siku mbili mara baada ya msafara wa timu hiyo utakapotua Botswana.


“Makusudi tumewatanguliza viongozi wetu watatu Botswana kwa ajili ya kuandaa mazingira mazuri ya timu itakapofikia.


“Kikubwa kutafuta hoteli na uwanja mzuri tutakaoutumia kwa ajili ya mazoezi vitu vyote hivyo vimepatikana.


“Tatizo lilikuwepo ni kwenye uwanja wa mazoezi pekee ambao tuliubadilisha haraka baada ya kuhisi hujuma kwa wapinzani wetu, hivyo tumetafuta mwingine tutakaoutumia kwa siku mbili pekee,” alisema mtoa taarifa huyo.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments