Recent-Post

MAKAMU MWENYEKITI WA CCM ZANZIBAR DK.SHEIN AONGOZA KIKAO CHA KAMATI MAALUM YA CCM ZANZIBAR AFISI KUU YA CCM KISIWANDUI



MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Zanzibar Rais Mstaafu wa Zanzibar Mhe.Dk.Ali Mohamed Shein akiongoza Kikao cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar, kilichofanyika katika ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar na (kulia kwake) Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambae pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Mhe Hemed Suleiman Abdulla.(Picha na Ikulu)


WAJUMBE wa Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar wakiwa katika ukumbi wa mkutano Afisi Kuu ya CCM Zanzibar, wakipitia makabrasha kabla ya kuaza kwa Kikao cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar, kilichofanyika leo kilichoongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Zanzibar Rais Mstaaf wa Zanzibar Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambae pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Zanzibar Dr. Abdalla Juma Mabodi na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Bi. Lela Burhani Ngozi, alipowasili katika viwanja vya Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar kuhudhuria Kikao cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar kilichofanyika leo 18-10-2021

Post a Comment

0 Comments