MAKAMU WA RAIS DKT. PHILIP MPANGO AKERWA NA UHARIBIFU WA MIUNDO MBINU MKOA WA PWANI

 

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. Philip Mpango amesema anakerwa na baadhi ya viongozi wa Chama Cha Mapinduzi Mkoani Pwani ambao wanatuhumiwa kuwa wanajihusisha kuhujumu miradi mikubwa ya kimkakati ya serikali ukiwemo mradi wa kufua umeme  wa bwawa  la Mwalimu  Julius Nyerere lililopo Rufiji Mkoa wa Pwani.
 
Makamu wa Rais Dkt. Mpango,  alisema hayo leo katika mkutano wake ambao umehitimisha ziara yake ya siku mbili  iliyofanyika kwenye ukumbi wa jengo la Wauguzi Kibaha, alipozungumza na Wajumbe wa Kamati za Siasa za Wilaya , Mkoa, Wabunge, na Madiwani wa Mkoa wa Pwani huku akisema kuwa amepata taarifa kuwa kuna baadhi ya viongozi wa CCM Mkoa wa Pwani ambao wamekua wakiwatuma vijana kuhujumu baadhi ya miradi mikubwa inayojengwa.

Aliitaja baadhi ya miradi  ambayo imeripotiwa kuhujumiwa  kuwa ni pamoja na mradi wa bandari kavu iliyopo Kwala  ambayo ni ujenzi wa reli ya Kisasa (SGR) , ambapo amepata ripoti kuwa wapo baadhi ya Viongozi wa CCM  wanahamasisha vijana kuharibu miundombinu hiyo ikiwa ni pamoja na wizi wa nondo ambazo huziuza   kama chuma chakavu huku akielekeza vyombo vya dola kuwashughulikia wote watakaokamatwa katika kujihusisha na hujuma hizo na kuwapa adhabu stahili.

"Ninazo taarifa kwamba kwenye bwawa la Mwalimu Nyerere (Stigler's Gorge) lililopo Wilayani Rufiji  wapo watu wanaiba mifuko  ya  saruji na kwenda kuiuza  mitaani jambo linalokwamisha kukamilika kwa wakati bwawa hilo"alisema Dkt. Mpango.

Aidha Dkt.Mpango alipokagua mradi wa jengo  la CCM Mkoa wa Pwani ambalo ujenzi wake umesimama kwa sasa aliwataka  viongozi kuorodhesha  mchanganuo wa gharama  za ujenzi uliofanyika hadi sasa na kuorodhesha gharama zonazohitajika Ili ujenzi ukamilike huku akitoa wiki mbili apatiwe ripoti kamili.

Aidha  katika harambee iliyofanyika Machi mwaka 2020 iliyongozwa na aliyekuwa Makamu wa Rais na Mlezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoani Pwani Mama Samia Suluhu kwa wakati huo ambapo ilielezwa ilikua ikihitaji Mil.500, katika harambee hiyo ilipatikana Milioni 584.1
Fedha taslimu Mil.113.4 na ahadi ilikua Mil.476.

Pia  katika harambee hiyo ilipatikana mifuko ya saruji 400 ndoo za rangi 50 ambapo Ofisi ya Makamu wa Rais kwa wakati huo ilichangia kiasi cha Mil.10.

Dkt. Mpango amesema atakapopata taarifa na kuridhishwa na tathmini ya namna fedha zilivyotumika ameahidi kutoa mifuko 500 ya saruji kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa jengo hilo .













TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments