Manula apewa ufalme Simba

 MAKIPA watatu waliopo ndani ya Simba wakae kwa akili Msimbazi, kwani Kocha Didier Gomes amefunguka na kuweka wazi kwamba kipa namba moja wake ni Aishi Manula na ataendelea kumpa nafasi kila mara kwa kiwango bora alichonacho licha ya kuwa na wengine kikosini.

Simba ina makipa manne, akiwamo Manula, Jeremiah Kisubu, Ally Salim na Beno Kakolanya, lakini juzi Kocha Gomes aliliambia Mwanaspoti kuwa, hawezi kufanya mabadiliko kwa kila mchezo ili makipa wake wapate nafasi, ila anachokiangalia ni uwezo wa kila mchezaji na ndipo anapata nafasi.

“Sidhanii kama nitakuwa na mabadiliko kwenye eneo la kipa kwani Manula amekuwa katika kiwango kizuri, ameonyesha ubora mechi za timu ya Taifa, hivyo ni ngumu sana kukaa nje,” alisema Gomes.

“Makipa wote waliopo ni wazuri, ila kwa anayepata nafasi ni kulingana na kiwango atakachokionyesha, Beno, Ally na Jeremiah wote wanakuja vizuri kwenye kikosi pia. Manula anajiamini sana, hiyo imetokana na kupata muda mwingi wa kucheza, kwani ni miongoni mwa makipa bora Afrika wanaofanya vizuri.”

Manula amekuwa katika kiwango kizuri kwa misimu mitatu mfululizo ambayo yote amekuwa kipa bora wa Ligi akiwa na kikosi cha Simba, akiwa pia ni kipa chaguo la kwanza kwenye timu hiyo.

Lakini msimu huu kwenye mazoezi ambayo yalikuwa yanaendelea katika uwanja wa Boko Veteran, makipa wote wa kikosi hicho wameonyesha kiwango bora hali ambayo ni kama watakuwa wanaviziana kupata namba.

Msimu uliopita Manula alimaliza ligi bila kuruhusu nyavu kuguswa mara 18.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments