MBEGU YA ALIZETI KUUZWA KILO MOJA TSH.3500/=

Waziri wa Kilimo, Prof. Adolf Mkenda akimkabidhi mfuko wa mbegu ya alizeti zilizozalishwa na Wakala wa Mbegu za Kilimo(ASA), Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Fatma Mganga wakati wa uzinduzi wa Mpango wa usambazaji wa mbegu za Alizeti nchini
Waziri wa Kilimo,Prof. Adolf Mkenda akiteta jambo na Dkt. Sophia Kashenge Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Mbegu za Kilimo(ASA)katikati, Kulia ni Mkuu wa Kitengo wa Mawasiliano Serikalini,Wizara ya Kilimo Bw. Hudson Kamoga
Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Mwanahamisi Munkundi
Waziri wa Kilimo, Prof. Adolf Mkenda akimkabidhi Mwenyekiti wa wakulima wa Alizeti Bw. Steven Maleale mfuko wa mbegu ya alizeti zilizozalishwa na Wakala wa Mbegu za Kilimo(ASA), wakati wa uzinduzi wa Mpango wa usambazaji wa mbegu za Alizeti nchini
Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Fatma Mganga (Kulia) na Mwenyekiti wa wakulima wa alizeti Bw. Steven Maleale baada ya kukabidhiwa mifuko ya mbegu na Waziri wa Kilimo, Prof. Adolf Mkenda kama ishara ya uzinduzi wa usambazaji wa mbegu ya alizeti nchini

..............................................

Mhe.Prof. Adolf Mkenda amezindua rasmi zoezi la Mpango wa usambazaji wa Mbegu za Alizeti kwa wakulima, huku akiagiza Mbegu hizo kuuzwa kwa kilo moja TSH.3,500 kwa wakulima.

Akizungumza na wakulima, pamoja na wadau wa zao la Alizeti katika ofisi ndogo za wizara ya kilimo,Kilimo4 mkoani Dodoma, waziri Mkenda amesema, serikali imeweka mkakati kuhakikisha changamoto ya Mbegu inakwisha kwa miaka michache ijayo.

Amesema kwa Mara ya kwanza serikali imetenga zaidi ya Tsh Bilioni 2.2 kwa ajili ya kuzalisha mbegu bora za alizeti karibu tani 2,000.

Waziri amewataka wafanya Biashara kuwekeza katika kilimo Cha Alizeti hasa katika Uzalishaji wa Mbegu ili waweze kupata fedha kwa haraka kutokana na uwepo wa soko la uhakika.

Ameongeza kuwa, mahitaji ya Mbegu za Alizeti ni makubwa hapa Nchini ambapo kwa Sasa zimepatikana Tani 1,600 Hadi 2000 huku mahitaji halisi yakiwa ni Tani 5,000.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Mbegu za kilimo ASA Dkt. Sophia Kashenge amesema, Kama Taasisi inaendelea kufuata maelekezo ya wizara ya kilimo na kuhakikisha changamoto ya Mbegu inakwisha.

Amesema, Mbegu hizo zitauzwa kwa shilingi 3,500 kwa kilo moja Kama waziri wa Kilimo alivyo agiza huku akiwataka wakulima kununua Mbegu hizo kwa Bei nafuu kutoka kwa Wakala wa serikali.

Naye Katibu Tawala wa mkoa wa Dodoma Dkt. Fatuma Mganga amesema, Kama mkoa wamejipanga kuhakikisha Mbegu hiyo ya Alizeti inawafikia wakulima kupitia Halmashauri zao kwa bei iliyoelekezwa na serikali.

Amesema, kupitia wakuu wa wilaya na wakurugenzi wa Halmashauri hizo ufanisi wa kilimo Cha Alizeti katika maeneo yao ndio itakuwa kipimo Chao Cha kazi, kuongeza kuwa hategemei Kama wilaya ama Halmashauri mojawapo itahindwa kufikia malengo.

Akimwakilisha Mkuu wa mkoa wa Dodoma Bi. Mwanahamisi Munkunda ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Bahi, amesema, maelekezo yote ya serikali yaliyotolewa juu ya Mbegu za Alizeti kwa wakulima yatafanyiwa kazi kulingana na umuhimu wake nakuongeza kuwa mkoa wa Dodoma Kama miongoni mwa mikoa ya kimkakati utafanya vizuri katika kilimo cha alizeti.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments